Ndugu wana taaluma ya Kinywa na Meno.
Salamu kutoka Chama Cha adaktari Wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA).

PRE-CONFERENCE ACTIVITY

Butiama Outreach November 26, 2018
JUMATATU Tar 26 Nov 2018 kutakuwa na Utoaji wa huduma za kinywa na meno bila malipo ktk kijiji cha Butiama ili kumuenzi Baba Wa Taifa Hayati Mwl. JULIUS K. NYERERE.

  • Wote ambao wanatarajia kushiriki ktk Utoaji wa huduma Butiama, lakini bado hawajathibitisha ushiriki wao wanaombwa kufanya hivyo.

CONFERENCE

The 33rd TDA Scientific Conference
TAR 28 HADI 30 NOV 2018 tutakuwa na Kongamano la 33 la Kisayansi na Mkutano Mkuu ufunguzi utafanywa na Mh. Ummy Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto. Kongamano litafungwa na Mh. Adam Kighoma Malima, Mkuu wa Mkoa Wa Mara.

  • Wale wote wanaotarajia kushiriki Kongamano hili tunaomba wajisajili kwa kuandika Majina kamili na cheo cha kitaaluma au kazi yako na Mkoa unaotoka.
  • Tunaombwa tutoe issues mbalimbali ambavyo tungependa vijadiliwe ktk Mkutano Mkuu (AGM)Tar 29 Nov 2018.
  • Kutakuwa na utaratibu wa usajili kwa uanachama wa TDA kama ambavyo Katiba Ya TDA ya Oktoba 2016 inavyoelekeza.

Taarifa zaidi za usajili na utaratibu mzima utawekwa ktk magroup yetu yote kuanzia kesho.